Akionekana ni mwenye ngozi nyororo na umbo lenye mvuto kama
mshambuliaji wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, kijana anaetambulika kwa
jina Joe Weller, amekua akiwahadaa wasichana kwa kujifafanisha na Cristiano
Ronaldo.
Kijana huyo amekuwa akifanya matukio ya kuwahadaa watu hususana
wasichama, katika mji wa Brighton uliopo kusini mwa Uingereza ambapo mara
kadhaa wasichana wamekua wakivutiwa nae na kufikia hatua ya kumtamani kutokana
na mvuto wake.
Hata hivyo wasichama wengi wamekuwa wakiamini kijana huyo ndio
Ronaldo wa ukweli, kutoka kwenye klabu ya Real Madrid kwa namna anavyovaa na
muonekano wake na pia hutumia matamshi ya maneno ya lugha ya kireno.
Mbali na hivyo wasichama wengine hufika mbali zaidi kwa kutaka
kumbusu na kumkumbatia ikiwa ni sehemu ya kutaka kuonyesha hisia zao kimapenzi
kwa Cristoano Ronaldo ambaye inasemakana hupata wakati mgumu anapokutana na
wakinadada mitaani.









No comments:
Post a Comment