Wednesday, October 1, 2014

Fabregas Na Filipe Luis Watupia Picha Za Shangwe la Ushindi Instagram.

Fabregas Na Filipe Luis Watupia Picha Za Shangwe la Ushindi Instagram

Kiungo kutoka nchini Hispania, Cesc Fabregas pamoja na beki wa pembeni kutoka nchini Brazil Filipe Luis wameanika picha za wachezaji wenzao wa klabu ya Chelsea katika mtandao wa kijamii wa Instagram kwa dhamira ya kuonyesha namna walivyokuwa na furaha mara baada ya kupata point tatu ugenini usiku wa kuamkia hii leo huko mjini Lisbon nchini Ureno.
Fabregas na Filipe Luis, walikuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea kilichoibuka na ushindi katika mchezo huo dhidi ya Sporting Lisbon, wameweka picha katika mtandao huo zikionyesha matukio tofauti ya furaha.
Picha ya Filipe Luis inaonyesha furaha iliyokuwa imekithiri miongoni mwa wachezaji wa Chelsea walipokuwa katika vyumba vya kubadilishia na picha ya Fabregas inaonyesha wachezaji wa Chelsea kwenye ndege tayari kwa safari ya kurejea jijini London nchini Uingereza.
Katika mchezo huo Chelsea walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na kiungo kutoka nchini Serbia, Nemanja Matic.

No comments:

Post a Comment

TEAM PARTICIPATING