Sunday, September 28, 2014

EPL: Liverpool vs Everton matokeo haya hapa.

article-2771838-21B5726C00000578-551_636x418
Nchini Uingereza mjini Liverpool leo kulikuwa mchezo wa wapinzani wa jadi kati ya majogoo wa jiji Liverpool dhidi ya Everton.
Wakiwa hawajawahi kushinda katika uwanja wa Anfield katika kipindi cha miaka 15 – Everton walijitupa katika uwanja wa wapinzani wao wakiwa na nia ya kuvunja rekodi mbovu waliyonayo kwenye uwanja huo, lakini alikuwa nahodha Steven Gerrard katika dakika ya 65 aliandikia timu ya Liverpool goli la kwanza kwa mkwaju wa faulo.
Huku dakika zikiwa zinayoyoma na mashabiki wa Liverpool wakia wamejiwekea uhakika wa kutamba mbele ya wapinzani wao, katika dakika ya 92 mlinzi wa kimataifa wa England Phil Jagielka  alifumua shuti kali  lilojaa kimiani na kuisawazishia Everton.
Timu zilipangwa hivi
Liverpool (4-2-3-1): Mignolet 5.5; Manquillo 7, Skrtel 7.5, Lovren 7, Moreno 7.5; Gerrard 8, Henderson 8.5; Sterling 8, Lallana 7.5, Markovic 5 (Coutinho 60); Balotelli 6 (Lambert 88)
Subs not used: Jones (GK), Enrique, Toure, Lambert, Coutinho, Lucas, Suso
Manager: Brendan Rodgers 7.5
Goal: Gerrard 64
Booked: Gerrard, Moreno
Everton (4-3-3): Howard 5.5; Hibbert 5.5 (Browning ’73), Stones 7, Jagielka 8, Baines 6.5; McCarthy 7, Barry 5.5, Besic 7 (Eto’o ’80); Lukaku 5, Naismith 6, Mirallas 6 (McGeady ’31)
Subs not used: Robles (GK), Gibson, Osman, Alcaraz
Manager: Roberto Martinez 6.5
Goal: Jagielka 90+1
Booked: Barry

EPL: Man City vs HulL City magoli na matokeo haya hapa

1411833819015_Image_galleryImage_HULL_ENGLAND_SEPTEMBER_27
Siku saba baada ya kutoshana nguvu na viongozi wa ligi Chelsea, vijana wa Manuel Pellegrini Manchester City leo walisafiri mpaka KC Stadium kucheza dhidi ya Hull City.
Iliwachukua dakika saba tu Manchester City kuandika goli la kwanza kupitia Sergio kun Aguero na muda mfupi baadae Edin Dzeko akaifungia City goli la pili kwa mkwaju mkali nje ya eneo la 18 la Hull City.
Vijana wa Steve Bruce wakapambana na kufanikiwa kupata goli la kwanza baada ya Eliaquim Mangala kujifunga wakati akizuia krosi ya hatari golini kwake dakika ya 21, na dakika 11 baadae Hull wakapata penati ambayo iliwekwa kimiani na Hernandez.
Mpaka mapumziko timu zilikuwa zimetoshana nguvu.
Kipindi cha pili magoli mawili ya Frank Lampard na Edin Dzeko kwa mara nyingine tena yakawapa ushindi wa 4-2 dhidi ya Hull City.
Timu zilipangwa
Hull City: McGregor 5.5; Rosenior 6.5, Dawson 6.5, Davies 6, Robertson 5.5 (Brady 83); Elmohamady 6, Diame 6.5, Huddlestone 6, Livermore 5.5 (Ben Arfa 74, 6); Hernandez 6.5 (Ramirez 74, 6), Jelavic 7 
Substitutes not used: Bruce, Chester, Harper, Quinn
Scorers: Mangala own goal 21; Hernandez pen 32
Manchester City: Caballero 5, Zabaleta 6.5, Mangala 4.5, Clichy 5.5, Kompany 6.5, Silva 7 (Demichelis 76, 6), Fernandinho 6 (Jesus Navas 66, 6), Yaya Toure 6.5, Milner 6, Aguero 6.5 (Lampard 71, 7), Dzeko 8
Substitutes not used: Hart, Sagna, Kolarov, Pozo
Scorers: Aguero 7; Dzeko 11, 68; Lampard 87
Booked: Mangala, Clichy
Referee: Anthony Taylor 6
Star man: Sergio Aguero 

EPL: Arsenal vs Tottenham – matokeo haya hapa.

article-2772055-21B7B7E300000578-576_636x444
Baada ya mchana wa leo kuhushudia ‘MersesydeDerby’ kati ya Liverpool dhidi ya Everton, muda mfupi uliopita huko London ya kaskazini mahsimu wengine wa EPL, Arsenal na Tottenham Hotspur walikuwa dimbani kushindania ufalme wa jiji hilo – North London Derby.
Mchezo huo uliokuwa mgumu na kasi kwa timu zote mbili umemalizika hivi punde katika uwanja wa Emirates na kuisha kwa matokeo ya sare ya 1-1.
Spurs walitangulia kufunga goli la kuongoza katika dakika ya 56 mfungaji akiwa Chadli, lakini mabadiliko ya Arsenal ya kumuingiza Alexis Sanchez yalichochea timu hiyo kupata goli la kusawazisha kupitia Chamberlain katika dakika ya 74.
Timu Zilipangwa kama ifuatavyo
Arsenal: Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta (Flamini 28), Oxlade-Chamberlain, Ramsey (Cazorla 45), Wilshere (Sanchez 63), Ozil, Welbeck.
Subs Not Used: Rosicky, Podolski, Ospina, Coquelin.
Booked: Oxlade-Chamberlain, Wilshere, Chambers.
Goals: Oxlade-Chamberlain 74.
Tottenham Hotspur: Lloris, Naughton, Kaboul, Vertonghen, Rose (Dier 83), Mason, Capoue, Lamela, Eriksen (Lennon 62), Chadli (Bentaleb 80), Adebayor.
Subs Not Used: Soldado, Vorm, Townsend, Fazio.
Booked: Lamela, Chadli, Adebayor, Lennon, Mason, Rose.
Goals: Chadli 56.
Att: 59,900
Ref: Michael Oliver (Northumberland).

EPL: Chelsea bado moto – hiki ndicho walichowafanya Aston Villa.

1411830758819_wps_6_Oscar_of_Chelsea_celebrat
Wiki moja baada ya kushindwa kupata ushindi kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye ligi kuu ya England, viongozi wa EPL klabu ya Chelsea leo waliwakaribisha Aston Villa katika uwanja wa Stamford Bridge.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa kwa vijana wa Jose Mourinho dhidi ya Villa ambao walipoteza mechi yao ya wiki iliyopita waliyocheza dhidi ya Arsenal.
Magoli ya Oscar, Willian na Diego Costa yalitosha kuwapa Chelsea ushindi wa magoli 3-0 na hivyo kuendelea kushika usukani mwa msimamo wa ligi hiyo ya England.
TIMU ZILIPANGWA HIVI
CHELSEA 4-2-3-1: Courtois 6.5; Ivanovic 7, Cahill 5.5, Terry 6, Azpilicueta 6; Fabregas 7, Matic 7; Willian 7.5, Oscar 7 (Mikel 77), Hazard 6 (Schurrle 68, 6); Costa 7 (Remy 81).
Subs not used: Cech, Luis, Zouma, Drogba, Remy.
Bookings: Cahill, Fabregas.
Manager: Jose Mourinho 7.
ASTON VILLA 4-5-1: Guzan 6.5; Hutton 6, Senderos 6, Baker 6, Cissokho 6; Richardson 6 (Bent 69, 5), Cleverley 6.5, Westwood 6.5, Delph 7, Weimann 5 (N’Zogbia 69, 5); Agbolahor 7.
Subs not used: Given, Clark, Bacuna, Sanchez, Grealish.
Bookings: Cleverley, Senderos
Manager: Paul Lambert 6

LaLiga: Matokeo ya Real Madrid vs Villareal na walichokifanya mashabiki wa Man United vyote viko hapa.

1411830960089_wps_25_Real_Madrid_s_Cristiano_R

Baada ya kuifumua Elche magoli 5-1 katikati mwa wiki hii, Real Madrid leo walisafiri mpaka katika dimba la EL Madrigal kukipiga dhidi ya Villareal katika mchezo wa kugombea uchampion wa ligi kuu ya Hispania – Laliga.
Wakicheza kwa kujihami Villareal waliruhusu nyavu zao kuguswa katika dakika ya 32 baada ya Luka Modric kuipatia Madrid goli la kuongoza.
Mwanasoka bora wa ulaya na dunia Cristiano Ronaldo kwa mara nyingine tena wiki hii akaifungia Madrid goli la pili katika dakika ya 40 ya mchezo huo.
Mpaka mwamuzi anapuliza kipenga Madrid walikuwa na ushindi wa 2-0 kibindoni.
1411833935717_wps_5_epa04420167_View_of_a_pla
Lakini wakati mchezo huo ukiendelea kikundi cha mashabiki wa Man UNited wanaojiita ‘United Reel’ walitimiza ahadi yao ya kurusha ndege juu ya uwanja huo huku ikiwa na ujumbe kwenye kwa Ronaldo kwamba arudi nyumbani Manchester.

EPL: Rooney aingusha timu yake, haya hapa matokeo ya Man U vs West Ham

article-2771941-21B6773E00000578-530_964x386
Ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena leo huku klabu ya Manchester United ikijitupa uwanjani kucheza dhidi ya West Ham katika kuusaka ushindi wa pili kwenye ligi hiyo tangu ilipoanza.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford, nahodha wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney alifanya makosa ya kizembe yaliyomsababishia kadi nyekundu ya moja moja baada ya kumkata mtama Stewart Downing na hivyo atakosa mechi 3 zijazo za premier league.
Pamoja na Rooney kuwaangusha wachezaji wenzie kwa kadi nyekundu ya kujitakia, lakini Manchester ilifanikiwa kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya vijana wa Sam Alladyce.
Rooney alianza kuifungia United goli dakika za mwanzo tu za mchezo na dakika kadhaa baadae Robin van Persie akaiandikia timu yake goli la pili.
West Ham walitulia na kujipanga vizuri na kufanikiwa kufunga goli lao moja kupitia Sakho baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Man United.
Man United walicheza kwa zaidi ya dakika 40 wakiwa pungufu baada ya Rooney kupewa kadi nyekundu.
TIMU ZILIPANGWA HIVI….
Manchester United (4-1-2-1-2): De Gea 6; Rafael 6, McNair 7, Rojo 6, Shaw 6; Blind 7; Herrera 7 (Valencia 74 6), Di Maria 6 (Thorpe 90 6); Rooney 4; Van Persie 7, Falcao 6 (Fletcher 65 6).
Sent off: Rooney.
Booked: Herrera.
West Ham (4-3-1-2): Adrian 5; Demel 6 (Jenkinson 65 6), Tomkins 6, Reid 5, Cresswell 6; Song 5, Poyet 6, Amalfitano 6 (Cole 61 6); Downing 6: Sakho 7, E Valencia 6.
Booked: Song, Sakho.
Referee: L Mason.
Man of the match: Blind.

Rekodi mpya ya Messi na matokeo ya FC Barcelona vs Granada.

1411839045997_wps_15_Barcelona_s_Brazilian_for
Akiwa na miaka 27 tu mwanasoka bora wa zamani wa dunia Lionel Messi amezidi kuchafua vitabu vya rekodi kwa kuweka na kuzivunja rekodi mwenyewe.
Leo hii wakati FC Barcelona ilipoikaribisha Granada kwenye dimba la Nou Camp, Lionel Messi alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 6-0.
Magoli hayo mawili yamemfanya Messi atimize jumla ya magoli 401 katika mechi 524 alizoichezea FC Barca na Argentina. Hii ni rekodi mpya kwa Messi.
Magoli mengine ya Barca yalifungwa na Neymar aliyefunga matatu, na Rakitic.
Timu ziliapangwa kama ifuatavyo
Barcelona: Bravo, Mathieu, Dani Alves, Adriano, Mascherano, Busquets (Bartra 64), Xavi, Rakitic (Sergi 58), Neymar, El Haddadi (Ramirez 71), Messi.
Subs not used: Ter Stegen, Montoya, Pedro, Iniesta.
Goals: Neymar 26,45 & 66, Rakitic 43, Messi 62 & 82.
Bookings: Dani Alves
Granada: Fernandez Alvalleros, Foulquier, Claude Babin, Nyom, Murillo, Yuste Canton (Pascual Israfilov 45), Marquez Moreno, Iturra, Rico Castro (Medina Luna 45), El-Arabi (Martins 73), Success Ajayi.
Subs not used: Olazábal Paredes, Mainz, Nounkeu, Cordoba.
Bookings: Rico Castro, Foulquier.
Referee: Juan Martínez Munuera
Attendance: 72,596

TEAM PARTICIPATING