Club Football Hot News

Wednesday, October 15, 2014

Cristiano Ronaldo awa staa wa pili kufikisha likes milioni 100 Facebook baada ya Shakira.

10334368_814560345274579_6152529128868119107_n
Mchezaji wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo amekuwa staa wa pili duniani baada ya Shakira kufikisha likes milioni 100 kwenye mtandao wa Facebook.
Ronaldo pia ni miongoni mwa wanamichezo mwenye followers wengi kwenye mtandao wa Twitter akiwa na milioni 30. Hii ni moja ya sababu inayomfanya mwanamichezo huyo kuingiza fedha nyingi zaidi kuliko wenzie hasa kwenye soka.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook wa mwanamichezo huyo ameandika: I’m so happy I reached 100 million friends on Facebook. It’s amazing! Thank you everyone.

Friday, October 10, 2014

Spain yapoteza mechi ya kwanza ya kufuzu Euro 2016 baada ya miaka 8.

s48

Timu ya taifa ya Hispania jana usiku ikiwa ugenini ikicheza mchezo wao kugombea kufuzu Euro 2016 dhidi ya Slovakia, ilijikuta ikifungwa katika kipindi cha kwanza kwa makosa ya kipa Iker Casillas aliyefanya uzembe wa ajabu na kuruhusu Slovakia kupata goli la kuongoza kupitia free-kick iliyoenda moja kwa moja ndani ya nyavu.
Katika dakika 83, mchezaji wa Spain, Paco Alcacer alisawazisha na mashabiki wengi wakajua mchezo huo utaisha kwa sare lakini goli la mchezaji wa zamani wa Chelsea na Rangers, Miroslav Stoch likaipa Slovakia ushindi katika dakika 87 dhidi ya mabingwa watetezi wa Ulaya.
Baada ya mchezo huo wachambuzi wa soka wamesema sasa inabidi apewe nafasi David De Gea na Iker Casillas apumzishwe. Hii ni mechi ya kwanza kwa Spain kupoteza katika hatua ya kufuzu michuano ya Ulaya au kombe la dunia katika kipindi cha miaka 8. Diego Costa bado hajafanikiwa kuifungia Spain goli tangu alipoamua kuitumikia timu hiyo.

Monday, October 6, 2014

Picha: Arsene Wenger na Jose Mourinho walivyotaka kuzichapa uwanjani.

1412517546264_wps_25_Chelsea_V_Arsenal_5_10_20




Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na mwenzake wa Chelsea, Jose Mourinho almanusra wageuke Mayweather na Maidana kwenye mechi kali iliyofanyika Stamford Bridge kati ya timu hizo.
Wakati mechi ikiendelea ikiendela palitokea kutokuelewana baina ya makocha hao wawili baada ya Wenger kumfuata Mourinho na kuanza kusukumana baada ya beki wa Chelsea, Cahil kumchezea rafu Sanchez.
1412518009731_wps_32_Chelsea_s_Portuguese_mana
Mwamuzi akijaribu kuwaamua
Makocha hao walijikuta wakianza kusukumana na nakutokea mzozo hadi mwamuzi alipowafuata na kuwapa onyo kuwa wakiendelea atawatoa wote nje ndipo walipotulia. Mchezo uliisha kwa Chelsea kushinda 2-0.
Akiongea na waandishi wa habari, Wenger alisema hajutii kitendo hicho.
1412518223101_Image_galleryImage_LONDON_ENGLAND_OCTOBER_05
Mzozo huo uliteka hisia za watu wengi
1412517666924_wps_30_Arsene_Wenger_manager_hea
Ubabe ubabe tu
1412517665657_Image_galleryImage_Arsene_Wenger_manager_hea

Wednesday, October 1, 2014

Video: Angalia Ronaldo Wa Bandia Anavyotamba Mitaani.

Video: Angalia Ronaldo Wa Bandia Anavyotamba Mitaani
Akionekana ni mwenye ngozi nyororo na umbo lenye mvuto kama mshambuliaji wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, kijana anaetambulika kwa jina Joe Weller, amekua akiwahadaa wasichana kwa kujifafanisha na Cristiano Ronaldo.
Kijana huyo amekuwa akifanya matukio ya kuwahadaa watu hususana wasichama, katika mji wa Brighton uliopo kusini mwa Uingereza ambapo mara kadhaa wasichana wamekua wakivutiwa nae na kufikia hatua ya kumtamani kutokana na mvuto wake.
 

Hata hivyo wasichama wengi wamekuwa wakiamini kijana huyo ndio Ronaldo wa ukweli, kutoka kwenye klabu ya Real Madrid kwa namna anavyovaa na muonekano wake na pia hutumia matamshi ya maneno ya lugha ya kireno.
Mbali na hivyo wasichama wengine hufika mbali zaidi kwa kutaka kumbusu na kumkumbatia ikiwa ni sehemu ya kutaka kuonyesha hisia zao kimapenzi kwa Cristoano Ronaldo ambaye inasemakana hupata wakati mgumu anapokutana na wakinadada mitaani.


Fabregas Na Filipe Luis Watupia Picha Za Shangwe la Ushindi Instagram.

Fabregas Na Filipe Luis Watupia Picha Za Shangwe la Ushindi Instagram

Kiungo kutoka nchini Hispania, Cesc Fabregas pamoja na beki wa pembeni kutoka nchini Brazil Filipe Luis wameanika picha za wachezaji wenzao wa klabu ya Chelsea katika mtandao wa kijamii wa Instagram kwa dhamira ya kuonyesha namna walivyokuwa na furaha mara baada ya kupata point tatu ugenini usiku wa kuamkia hii leo huko mjini Lisbon nchini Ureno.
Fabregas na Filipe Luis, walikuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea kilichoibuka na ushindi katika mchezo huo dhidi ya Sporting Lisbon, wameweka picha katika mtandao huo zikionyesha matukio tofauti ya furaha.
Picha ya Filipe Luis inaonyesha furaha iliyokuwa imekithiri miongoni mwa wachezaji wa Chelsea walipokuwa katika vyumba vya kubadilishia na picha ya Fabregas inaonyesha wachezaji wa Chelsea kwenye ndege tayari kwa safari ya kurejea jijini London nchini Uingereza.
Katika mchezo huo Chelsea walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri lililofungwa na kiungo kutoka nchini Serbia, Nemanja Matic.

Arsene Wenger Ni kiboko ya Mameneja 207 Wa Ligi Ya England Kwa Miaka 18.

Arsene Wenger Ni kiboko ya Mameneja 207 Wa Ligi Ya England Kwa Miaka 18

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger hii leo ametimiza miaka 18 kamili tangu alipoanza kuitumikia klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London oktoba mosi mwaka 1996.
Wenger, anatimiza miaka 18 huku hii leo kikosi chake kikikabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Galatasaray kutoka nchini Urutuki ambapo itamlazimu kufanya jitihada za kuinogesha furaha ya kuwa klabuni hapo kwa muda mrefu kwa kikosi chake kusaka ushindi.
Uwepo wa meneja huyo kutoka nchini Ufaransa, unaendelea kumpa sifa ya tofauti katika ligi ya nchini Uingereza kutokana na kuwa mtu aliyedumu kibaruani kwa kipindi kirefu huku klabu nyingine zikifanya mabadiliko ya mara kwa mara katika mabenchi yao ya ufundi.
Tangu mwaka 1996 Arsene Wenger, akiwa meneja wa klabu ya Arsenal klabu nyingine 43 zilizoshiriki ligi tangu kipindi hicho zimebadilisha jumla ya mameneja 207 na kumuacha akiwa meneja pekee anaebaki kuwa kiongozi wa benchi la ufundi la The Gunners.
Kwa mantiki hiyo sasa Arsene Wenger, anaendelea kuwa meneja aliyedumu Arsenal kwa kipindi kirefu kuliko meneja mwingine yoyote aliyepita klabuni hapo na pia anakuwa meneja aliyekaa kwa kipindi kirefu zaidi ya wengine katika ligi ya nchini Uingereza baada ya kuondoka kwa Sir Alex Ferguson aliyekuwa akikinoa kikosi cha Man Utd.
Arsene Wenger alitambulishwa rasmi kuwa meneja wa klabu ya Arsenal Oktoba mosi mwaka 1996, baada ya kukamilisha mipangop ya kusaini mikataba na viongozi wa klabu hiyo Septemba 30 mwaka huo.

Sunday, September 28, 2014

EPL: Liverpool vs Everton matokeo haya hapa.

article-2771838-21B5726C00000578-551_636x418
Nchini Uingereza mjini Liverpool leo kulikuwa mchezo wa wapinzani wa jadi kati ya majogoo wa jiji Liverpool dhidi ya Everton.
Wakiwa hawajawahi kushinda katika uwanja wa Anfield katika kipindi cha miaka 15 – Everton walijitupa katika uwanja wa wapinzani wao wakiwa na nia ya kuvunja rekodi mbovu waliyonayo kwenye uwanja huo, lakini alikuwa nahodha Steven Gerrard katika dakika ya 65 aliandikia timu ya Liverpool goli la kwanza kwa mkwaju wa faulo.
Huku dakika zikiwa zinayoyoma na mashabiki wa Liverpool wakia wamejiwekea uhakika wa kutamba mbele ya wapinzani wao, katika dakika ya 92 mlinzi wa kimataifa wa England Phil Jagielka  alifumua shuti kali  lilojaa kimiani na kuisawazishia Everton.
Timu zilipangwa hivi
Liverpool (4-2-3-1): Mignolet 5.5; Manquillo 7, Skrtel 7.5, Lovren 7, Moreno 7.5; Gerrard 8, Henderson 8.5; Sterling 8, Lallana 7.5, Markovic 5 (Coutinho 60); Balotelli 6 (Lambert 88)
Subs not used: Jones (GK), Enrique, Toure, Lambert, Coutinho, Lucas, Suso
Manager: Brendan Rodgers 7.5
Goal: Gerrard 64
Booked: Gerrard, Moreno
Everton (4-3-3): Howard 5.5; Hibbert 5.5 (Browning ’73), Stones 7, Jagielka 8, Baines 6.5; McCarthy 7, Barry 5.5, Besic 7 (Eto’o ’80); Lukaku 5, Naismith 6, Mirallas 6 (McGeady ’31)
Subs not used: Robles (GK), Gibson, Osman, Alcaraz
Manager: Roberto Martinez 6.5
Goal: Jagielka 90+1
Booked: Barry

EPL: Man City vs HulL City magoli na matokeo haya hapa

1411833819015_Image_galleryImage_HULL_ENGLAND_SEPTEMBER_27
Siku saba baada ya kutoshana nguvu na viongozi wa ligi Chelsea, vijana wa Manuel Pellegrini Manchester City leo walisafiri mpaka KC Stadium kucheza dhidi ya Hull City.
Iliwachukua dakika saba tu Manchester City kuandika goli la kwanza kupitia Sergio kun Aguero na muda mfupi baadae Edin Dzeko akaifungia City goli la pili kwa mkwaju mkali nje ya eneo la 18 la Hull City.
Vijana wa Steve Bruce wakapambana na kufanikiwa kupata goli la kwanza baada ya Eliaquim Mangala kujifunga wakati akizuia krosi ya hatari golini kwake dakika ya 21, na dakika 11 baadae Hull wakapata penati ambayo iliwekwa kimiani na Hernandez.
Mpaka mapumziko timu zilikuwa zimetoshana nguvu.
Kipindi cha pili magoli mawili ya Frank Lampard na Edin Dzeko kwa mara nyingine tena yakawapa ushindi wa 4-2 dhidi ya Hull City.
Timu zilipangwa
Hull City: McGregor 5.5; Rosenior 6.5, Dawson 6.5, Davies 6, Robertson 5.5 (Brady 83); Elmohamady 6, Diame 6.5, Huddlestone 6, Livermore 5.5 (Ben Arfa 74, 6); Hernandez 6.5 (Ramirez 74, 6), Jelavic 7 
Substitutes not used: Bruce, Chester, Harper, Quinn
Scorers: Mangala own goal 21; Hernandez pen 32
Manchester City: Caballero 5, Zabaleta 6.5, Mangala 4.5, Clichy 5.5, Kompany 6.5, Silva 7 (Demichelis 76, 6), Fernandinho 6 (Jesus Navas 66, 6), Yaya Toure 6.5, Milner 6, Aguero 6.5 (Lampard 71, 7), Dzeko 8
Substitutes not used: Hart, Sagna, Kolarov, Pozo
Scorers: Aguero 7; Dzeko 11, 68; Lampard 87
Booked: Mangala, Clichy
Referee: Anthony Taylor 6
Star man: Sergio Aguero 

EPL: Arsenal vs Tottenham – matokeo haya hapa.

article-2772055-21B7B7E300000578-576_636x444
Baada ya mchana wa leo kuhushudia ‘MersesydeDerby’ kati ya Liverpool dhidi ya Everton, muda mfupi uliopita huko London ya kaskazini mahsimu wengine wa EPL, Arsenal na Tottenham Hotspur walikuwa dimbani kushindania ufalme wa jiji hilo – North London Derby.
Mchezo huo uliokuwa mgumu na kasi kwa timu zote mbili umemalizika hivi punde katika uwanja wa Emirates na kuisha kwa matokeo ya sare ya 1-1.
Spurs walitangulia kufunga goli la kuongoza katika dakika ya 56 mfungaji akiwa Chadli, lakini mabadiliko ya Arsenal ya kumuingiza Alexis Sanchez yalichochea timu hiyo kupata goli la kusawazisha kupitia Chamberlain katika dakika ya 74.
Timu Zilipangwa kama ifuatavyo
Arsenal: Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta (Flamini 28), Oxlade-Chamberlain, Ramsey (Cazorla 45), Wilshere (Sanchez 63), Ozil, Welbeck.
Subs Not Used: Rosicky, Podolski, Ospina, Coquelin.
Booked: Oxlade-Chamberlain, Wilshere, Chambers.
Goals: Oxlade-Chamberlain 74.
Tottenham Hotspur: Lloris, Naughton, Kaboul, Vertonghen, Rose (Dier 83), Mason, Capoue, Lamela, Eriksen (Lennon 62), Chadli (Bentaleb 80), Adebayor.
Subs Not Used: Soldado, Vorm, Townsend, Fazio.
Booked: Lamela, Chadli, Adebayor, Lennon, Mason, Rose.
Goals: Chadli 56.
Att: 59,900
Ref: Michael Oliver (Northumberland).

EPL: Chelsea bado moto – hiki ndicho walichowafanya Aston Villa.

1411830758819_wps_6_Oscar_of_Chelsea_celebrat
Wiki moja baada ya kushindwa kupata ushindi kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye ligi kuu ya England, viongozi wa EPL klabu ya Chelsea leo waliwakaribisha Aston Villa katika uwanja wa Stamford Bridge.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa kwa vijana wa Jose Mourinho dhidi ya Villa ambao walipoteza mechi yao ya wiki iliyopita waliyocheza dhidi ya Arsenal.
Magoli ya Oscar, Willian na Diego Costa yalitosha kuwapa Chelsea ushindi wa magoli 3-0 na hivyo kuendelea kushika usukani mwa msimamo wa ligi hiyo ya England.
TIMU ZILIPANGWA HIVI
CHELSEA 4-2-3-1: Courtois 6.5; Ivanovic 7, Cahill 5.5, Terry 6, Azpilicueta 6; Fabregas 7, Matic 7; Willian 7.5, Oscar 7 (Mikel 77), Hazard 6 (Schurrle 68, 6); Costa 7 (Remy 81).
Subs not used: Cech, Luis, Zouma, Drogba, Remy.
Bookings: Cahill, Fabregas.
Manager: Jose Mourinho 7.
ASTON VILLA 4-5-1: Guzan 6.5; Hutton 6, Senderos 6, Baker 6, Cissokho 6; Richardson 6 (Bent 69, 5), Cleverley 6.5, Westwood 6.5, Delph 7, Weimann 5 (N’Zogbia 69, 5); Agbolahor 7.
Subs not used: Given, Clark, Bacuna, Sanchez, Grealish.
Bookings: Cleverley, Senderos
Manager: Paul Lambert 6

TEAM PARTICIPATING